“Boss amemganda Dangote,ameisahau Tip Top” kutoka kwa Roma ni moja kati ya mistari inayozungumziwa sana kwa sasa huku ikidaiwa kuwa Roma amemponda Babu Tale ambaye ni mmoja wa mameneja wa Diamond na meneja wa Tip Top pia kwenye wimbo wake wa kaa tayari.
Kwa
upande wake Roma amesema kuwa hakumaanisha kumponda meneja huyo kama
watu wengi wanavyodhani bali alitaka kufikisha ujumbe kuwa watu
wasisahau walipotoka lakini kwa njia ya kisanii zaidi.
“Tafsiri
ya mstari huo ni kwamba tusisahau tulipotoka,ningeweza tu kuandika
hivyo lakini kama msanii inabidi niwe mbunifu,ndio nikajenga hiyo picha
na ndiyo maana watu wameukumbuka zaidi” alifafanua Roma alipokuwa akihojiwa na HZB TV.
No comments:
Post a Comment