Sunday, July 24, 2016

Ali Kiba Afunguka Sababu za Kuwatosa Wanawake Watatu Alio zaa Nao....



Alikiba ameitaja sababu iliyomfanya ashindwe kumuoa mwanamke yeyote kati ya watatu aliozaa nao.

Hitmaker huyo wa Lupela alikiambia kipindi cha Chill na Sky kuwa hakupenda kulazimisha iwe hivyo.“Unajua hauwezi kumuoa mtu kama hamuelewani.

 Nia yangu ilikuwa ni kustick na kila mama wa mmoja toka nilipoanza. Lakini mambo yanaenda tofauti, huenda mnagombana anapata mtu mwingine,” anasema Kiba.“Kwahiyo hautakiwi kuforce mapenzi, mimi nataka nikae na mtu ambaye tutaelewana,” ameongeza.

Alikiba ana watoto wawili wa kike, Amiya Kiba, Chamy Kiba na mmoja wa kiume, Sameer Kiba. Wote ni watoto wa mama tofauti. 

No comments:

Post a Comment